| |
Hapa ni katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga ambapo leo Warembo 20 wanaoshiriki shindano la kutafuta mrembo wa mkoa wa Shinyanga(Miss Shinyanga 2014) wakiongozwa na mwandaaji wa Mashindano hayo bi Asela Magaka wa Asela Promotions wametembelea kituo na kutoa msaada wa vyakula huku wakichangia kidogo walichokuwa nacho kwenye mifuko yao kuchangia ujenzi wa bweni katika kituo hicho chenye watoto zaidi ya 260.Pichani ni baadhi ya warembo wakiwa na baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wakionesha upendo.
Misaada iliyotolewa na Asela Promotions na kukabidhiwa kwa mkuu wa kitengo cha Walemavu katika kituo cha Buhangija Jumuishi mwalimu Bright Mduma ni pamoja na,chumvi katoni 1, mchele kilo 100,unga wa sembe kilo 200,sukari kilo 20,mafuta ya kupikia lita 10,unga wa ngano kilo 50 na sabuni za unga za kufulia kilo 30, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 506,700/=