EWURA YAPUNGUZA GHARAMA ZA UWEKEZAJI VITUO VYA MAFUTA VIJIJINI

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeendelea kuchukua hatua za kupunguza gharama za uwekezaji katika vituo vya mafuta vilivyojengwa maeneo ya vijijini, kwa lengo la kuhamasisha wawekezaji na kuongeza upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kwa wananchi.

Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Nyarabu Msira, amesema kupunguzwa kwa gharama za uwekezaji kunalenga kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na wawekezaji kuanzisha vituo vya mafuta katika maeneo ambayo huduma hiyo bado haijafika kwa kiwango kinachohitajika.

Amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za kuhakikisha wananchi waishio vijijini wanapata huduma ya mafuta kwa urahisi na kwa ukaribu, sambamba na kuchochea shughuli za kiuchumi zinazotegemea nishati hiyo, ikiwemo usafirishaji, kilimo, biashara na huduma mbalimbali za kijamii.

Mhandisi Msira amewataka wawekezaji kutumia fursa hiyo kuwekeza katika maeneo ya vijijini huku wakizingatia sheria, kanuni na viwango vinavyowekwa na EWURA ili kuhakikisha vituo vinavyojengwa vinakuwa salama, vinatoa huduma bora na vinakidhi mahitaji ya wananchi. 

TAZAMA VIDEO👇👇


Post a Comment