.jpeg)
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umepongezwa kwa kuendelea kuboresha huduma za fidia, hususan kupitia matumizi ya mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), hatua inayolenga kuongeza ufanisi katika kushughulikia madai ya wafanyakazi wanaopata ajali, magonjwa au changamoto zinazohusiana na mazingira ya kazi.
Pongezi hizo zimetolewa na waziri wanchi ofisi ya waziri wa kazi ajira na mahusiano ya kazi Deusi Sangu wakati wa ushiriki wa WCF katika Maonyesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika Mkoani Geita, ambapo imeelezwa kuwa sekta ya madini ni miongoni mwa sekta muhimu katika uchumi wa Tanzania, ikichangia takribani asilimia 10.1 ya Pato la Taifa na kuajiri idadi kubwa ya Watanzania, hivyo umuhimu wa huduma za fidia kwa wafanyakazi katika sekta hiyo unaendelea kuongezeka.
Sangu amesema kuwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwake, WCF imeendelea kuimarisha mifumo ya utoaji huduma, ikiwemo matumizi ya TEHAMA katika kushughulikia madai na malalamiko.
Hatua hiyo inalenga kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wafanyakazi na waajiri, huku thamani ya mfuko ikitajwa kuongezeka kutoka takribani Sh bilioni 770 hadi zaidi ya Sh trilioni 1.1.
Tazama Video hapa Waziri Sangu akizungumza
