
Wakaguzi wa Migodi wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu na kuzingatia usalama ili kupunguza ajali zinazoweza kutokea kwenye shughuli za uchimbaji Madini.
Wito huo umetolewa na kamanda wa polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi alipokuwa akizungumza na wachimbaji wadogo wa Mgodi wa mwime uliopo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Hatua hiyo inalenga kuhakikisha shughuli za uchimbaji zinafanyika katika mazingira salama , yanayozingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kwa ajili ya kulinda maisha ya wachimbaji pamoja na watu wengine wanaofanya shughuli hizo.
Magomi amewataka wakaguzi kufanya ukaguzi wa kina kwenye maduara na kwenye maeneo yote ya mgodi ili kubaini mapungufu yanayoweza kusababisha ajali, ikiwemo kutokuzingatia taratibu za kiusalama ,na kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa kwa mujibu wa sheria.
"Tunataka wachimbaji waende salama kazini na warudi salama nyumbani
".amesema magomi
Amesisitiza wakaguzi kuhakikisha wanatenda haki kwa wachimbaji wa Madini na wadau wa sekta hiyo bila upendeleo,huku wakitoa elimu na ushauri juu ya umuhimu wa kuzingatia usalama wakati wote wa shughuli za uchimbaji.
Magomi amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha usimamizi wa sekta ya Madini na kujenga utamaduni wa usalama migodini ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na ajali na kulinda maisha ya wachimbaji.
Kwa upande wake Meneja mgodi wa mwime two Peter Nkarango amesema mgodi huo una wiki mbili tangu umefumuka na wamejipanga kuhakikisha maeneo ya kazi yanazingatia matakwa ya usalama.
Mkaguzi mkuu wa mgodi wa Mwime two amesema wanajumla ya duara 300 na duara zinafugwa matimba na kuwa imara ,na zoezi la ukaguzi wa maduara linafanyika usiku na mchana ili kuzuia ajali zisizo za lazima na kuwezesha wachimbaji kufanya kazi kwenye mazingira salama.


.jpeg)


.jpeg)

