WAKAGUZI WA MIGODI WATAKIWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA WELEDI


               Na Neema Sawaka,Kahama

Wakaguzi wa Migodi  wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu  na kuzingatia usalama ili kupunguza  ajali zinazoweza  kutokea  kwenye shughuli za uchimbaji Madini.

Wito huo umetolewa   na kamanda wa polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth  Magomi alipokuwa  akizungumza na wachimbaji wadogo wa   Mgodi wa mwime  uliopo wilayani Kahama  Mkoani Shinyanga.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha  shughuli za uchimbaji  zinafanyika  katika mazingira salama , yanayozingatia  sheria,  kanuni na taratibu zilizowekwa kwa ajili ya kulinda maisha ya wachimbaji pamoja na watu wengine  wanaofanya  shughuli hizo.

  Magomi    amewataka wakaguzi kufanya  ukaguzi wa kina kwenye maduara    na kwenye maeneo yote ya   mgodi   ili kubaini   mapungufu  yanayoweza kusababisha ajali,  ikiwemo kutokuzingatia  taratibu za kiusalama ,na kuhakikisha  hatua stahiki zinachukuliwa  kwa  mujibu wa sheria.

"Tunataka wachimbaji   waende salama kazini  na warudi salama nyumbani

".amesema  magomi

Amesisitiza  wakaguzi kuhakikisha  wanatenda haki  kwa  wachimbaji  wa  Madini   na wadau  wa sekta hiyo bila upendeleo,huku wakitoa  elimu na ushauri juu ya umuhimu  wa kuzingatia usalama wakati wote wa shughuli za uchimbaji.

Magomi amesema  hatua hiyo  inalenga  kuimarisha  usimamizi wa sekta ya Madini na kujenga  utamaduni  wa usalama  migodini ili kupunguza  madhara  yanayoweza kujitokeza kutokana na  ajali  na kulinda  maisha ya wachimbaji.

Kwa upande wake Meneja mgodi wa mwime two  Peter Nkarango amesema  mgodi huo una wiki mbili  tangu umefumuka  na  wamejipanga  kuhakikisha maeneo ya kazi yanazingatia  matakwa  ya usalama.

Mkaguzi  mkuu wa mgodi wa Mwime two  amesema  wanajumla ya  duara 300 na duara  zinafugwa matimba na  kuwa imara ,na zoezi la ukaguzi wa maduara  linafanyika  usiku na mchana  ili kuzuia  ajali zisizo za  lazima na kuwezesha  wachimbaji kufanya kazi kwenye mazingira  salama.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi akizungumza na wachimbaji wadogo

 

Post a Comment