SACP MWAMBELO ATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI, ABAINI UKIUKWAJI WA SHERIA

       Mnadhimu wa Polisi Kitengo cha usalama barabarani SACP Butusyo Mwambelo akizungumza na abiria katika stend ya mabasi Shinyanga
           

Imeelezwa kuwa asilimia kubwa ya ajali za barabarani nchini husababishwa  na makosa ya kibinadam ambayo iwapo yatazingatiwa na kuchukuliwa maanani yanaweza kupunguza kiwango kikubwa cha  ajali hizo.

Mnadhimu wa Polisi Kitengo cha usalama barabarani SACP Butusyo Mwambelo amesema hayo katika ukaguzi  na utoaji wa elimu ya usalama barabarani anayoifanya maeneo mbalimbali nchini.

Akiwa katika kituo cha mabasi cha Mkoa wa Shinyanga  na kituo kidogo kilichopo soko kuu,  Mwambelo amesema kuwa uzembe wa watumiaji wa Barabara hususani waendesha vyombo vya moto ndiyo chanzo cha ajali nyingi nchini ambapo katika ukaguzi huo amebaini changamoto ya makondakta kutotoa tiketi mtandao Pamoja na kutembea umbali mrefu pasipo kutoa tiketi.
 
SACP Mwambelo ametumia nafasi hiyo kutoa elimu kwa abiria, madereva, mawakala na waendesha pikipiki pamoja na madereva bajaji ikiwa ni sehemu ya kuimarisha suala zima la uzingatiaji wa sheria za usalama barabarani.

Naye ASP Mwashamba Onesmo kutoka makao makuu , amewataka madereva kutumia udereva wa kujiahami ili kuepuka ajali zinazoepukika na kuhakikisha wanaishi katika kauli mbiu isemayo-familia yako inakusubiri safiri salama.

 Mmoja wa abiria alieyekuwa akisafiri na basi la kampuni ya Asante rabi Daniel John-amesema  licha ya kupanda basi hilo kutokea Misungwi hadi  Shinyanga alikuwa hajapewa teketi yake kinyume cha utaratibu na sheria inanvyotaka. 

Naye dereva wa basi hilo Seif Shaban-amesema kuwa kufanya hivyo ni kunyume cha utaratibu na ni vema kondakta akafuata sheria ili kuepuka usumbufu  ambapo hali hiyo imepelekea kupigwa faini kwa kushindwa kukatisha tiketi abiria wake 
Ukaguzi na operation hiyo umefanyika leo  December 13, 2025 katika kituo cha mabasi shinyanga maarufu manyoni na stand ya soko kuu mjini Shinyanga ikilenga kutoa elimu kwa watumaiaji wa vyombo vya moto.

     

        Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi akimkaribisha Mnadhimu wa Polisi Kitengo cha usalama barabarani SACP Butusyo Mwambelo  




















 



Post a Comment