.jpeg)

Na Johnson James, KISHAPU
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, ameonesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Masagala, kinachojengwa katika Kijiji cha Masagala, Kata ya Maganzo, Wilaya ya Kishapu, kwa ufadhili wa Kampuni ya Mwadui kupitia mpango wa Uwajibikaji wa Makampuni kwa Jamii (CSR) na nguvu za wananchi.
Akizungumza Januari 10, 2026, wakati wa ziara ya kukagua hatua za utekelezaji wa ujenzi huo, Mhe. Mhita alisema mradi huo ni mfano bora wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na jamii katika kuimarisha huduma za afya na kupunguza adha kwa wananchi.
“Nimeridhishwa sana na kasi na ubora wa ujenzi wa kituo hiki. Hii ni jitihada kubwa na ya kuigwa, kwani wananchi walikuwa wanatembea hadi kilomita 20 kufuata huduma za afya,” alisema RC Mhita.
Awali, akitoa taarifa mwakilishi wa Mgodi wa WDL Sylivia Mulogo amesema jumla ya shilingi milioni 177 zinatarajiwa kutumika hadi kukamilika kwa kituo hicho. Majengo yanayojengwa ni OPD, Maabara, RCH, kichomea taka, na vyoo vya matundu matano.

Mkazi wa kijiji hicho, Bi. Doroth Balibusa, alisema wanawake wajawazito wamekuwa wakikumbwa na changamoto ya kujifungulia njiani, lakini sasa wana matumaini makubwa baada ya huduma kuletwa karibu nao.
Kituo cha Afya Masagala kinatarajiwa kukamilika ifikapo Februari 2026 na kuhudumia zaidi ya wananchi 22,000 kutoka vijiji vya jirani. .jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

