GEITA GIRLS YATAJWA KUKUZA NDOTO ZA WASICHANA KUPITIA ELIMU YA SAYANSI,WAPONGEZA JUHUDI ZA SERIKALI

Mkuu wa Shule ya Wasichana ya Geita, Mwamini Kagoma

Na Editha Edward,Geita

Katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Mkuu wa Shule ya Wasichana ya Geita, Mwamini Kagoma, anajivunia kuwa mwanamke shupavu na mama mlezi bora kwa watoto wa kike.
Akizungumzza leo Machi 8,2026 Shule ya Wasichana Geita (Geita Girls), Mwamini ameeleza kuwa shule hiyo ni miongoni mwa shule 26 za sayansi zilizojengwa nchini kwa juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Amewapongeza wanawake wote kwa juhudi zao katika kujenga jamii na kuleta maendeleo

Lengo la kuanzishwa kwa shule hizi ni kuinua na kuimarisha elimu kwa watoto wa kike kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita, ili kuwajengea uwezo wa kuwa viongozi bora wa baadaye.

“Ukimuelimisha mtoto wa kike, umeielimisha jamii, familia moja moja, na taifa kwa ujumla amesisitiza kuwa elimu ya mtoto wa kike ina mchango mkubwa katika maendeleo ya Jamii ”amesisitiza Mwamini
Kupitia shule ya Geita Girls, wanafunzi wanapatiwa mazingira bora ya kujifunza, hasa katika masomo ya sayansi, ili kuwasaidia kufikia ndoto zao na kuwa wanawake wenye mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi.

Post a Comment