TAMASHA LA AMANI NA MAENDELEO LATUMIKA KUIMARISHA UMOJA, VIPAJI NA UZALENDO

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Peter Masindi na Mbunge wa Jimbo la Kishapu Peter Masindi wakicheza draft wakati wa tamasha la amani na maendeleo katika uwanja wa shule ya msingi Buduhe.

 

Wilaya ya Kishapu imeendelea kudhihirisha dhamira yake ya kulinda amani na kusukuma mbele maendeleo kupitia Tamasha la Amani na Maendeleo, lililotumika kama jukwaa la kuwakutanisha wananchi, kukuza vipaji na kuimarisha mshikamano wa kijamii. Tamasha hilo limebeba ujumbe mzito wa uzalendo, likisisitiza kuwa maendeleo ya kweli hayawezi kupatikana bila amani na umoja.

Akizungumza katika tamasha hilo, Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Lucy Thomas Mayenga, amewahimiza wananchi kudumisha umoja na mshikamano, akibainisha kuwa amani iliyopo ni mtaji mkubwa wa maendeleo ya wilaya na taifa kwa ujumla.

Amesema tamasha hilo ni fursa adhimu ya kuimarisha mahusiano mema miongoni mwa wananchi na kuibua vipaji vipya, hususan kwa vijana na  amesisitiza kuwa uzalendo unapaswa kupewa kipaumbele katika kila hatua ya maendeleo.

Amesema  kuwa wananchi wanaposhirikiana bila migawanyiko ya kijamii au kisiasa, hujenga msingi imara wa maendeleo endelevu,ambapo  michezo na sanaa ni nyenzo muhimu za kuwaunganisha watu na kuwajengea nidhamu, afya na mshikamano.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga na mwandaaji wa Tamasha la Amani na Maendeleo Mhe. Peter Masindi akizungumza kwenye kilele cha tamasha hilo lililoanza Februari 23 hadi 28,2026 katika viwanja vya michezo shule ya msingi Buduhe iliyoko Kata ya Kishapu Wilayani humo

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Peter Masindi, amesema tamasha hilo lina mchango mkubwa katika kujenga afya za wananchi na kuinua vipaji vya vijana ,ambapo  Serikali inaendelea kuunga mkono jitihada za kukuza michezo kama njia ya kuwawezesha vijana kujitambua na kutumia vipaji vyao kama fursa ya maendeleo ya baadaye.

Mkuu wa Wilaya Masindi amewahimiza wazazi na walezi kuwaruhusu watoto wao kushiriki kikamilifu katika michezo na burudani mbalimbali, akisisitiza kuwa ushiriki huo huwasaidia vijana kujiamini, kuimarisha afya na kufungua milango ya fursa za kiuchumi kupitia michezo.

Tamasha hilo limeambatana na michezo na burudani mbalimbali zilizovutia makundi yote ya jamii, ikiwemo michezo ya karata na bao, mashindano ya kukimbiza kuku, kuvuta kamba, mpira wa miguu, mbio za kukimbia pamoja na ngoma za asili zilizopamba jukwaa na kuongeza hamasa kwa washiriki na watazamaji.

Kwa ujumla, Tamasha la Amani na Maendeleo Kishapu limeendelea kuwa mfano wa namna michezo na burudani vinavyoweza kutumika kuimarisha amani, kuibua vipaji na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa kuzingatia misingi ya umoja, mshikamano na uzalendo

Katibu Tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na Fatma Mohamed akizungumza kwenye kilele cha Tamasha la Amani na Maendeleo  lililoanza Februari 23 hadi 28,2026 .

Mwenyekiti wa Halmashauri Josephat Limbe, ameeleza kuwa michezo ni sekta inayokua kwa kasi na inaweza kuwa chanzo kikubwa cha ajira endapo itawekewa mikakati madhubuti na kuungwa mkono na wadau mbalimbali. Aliahidi kuwa Halmashauri itaendelea kuboresha miundombinu ya michezo na kuandaa mashindano mara kwa mara ili kuwapa vijana fursa zaidi

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Severine Msyangi, akiwa kwenye kilele cha Tamasha la Amani na Maendeleo.

  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Shija Ntelezu, akiwa kwenye kilele cha Tamasha la Amani na Maendeleo  lililoanza Februari 23 hadi 28,2026 katika viwanja vya michezo shule ya msingi Buduhe iliyoko Kata ya Kishapu Wilayani humoMkazi wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Pili Mazoya, akizungumzia tamasha hilo Februari 28,2026Mkazi wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Jitili Deus Kasekwa akizungumzia Tamasha hilo Februari 28,2026





















































































Post a Comment