Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wilaya ya Shinyanga, Leonard Waziri.
Wachimbaji wadogo wa madini katika Mgodi wa Mwakitolyo, Halmashauri ya
Shinyanga wamesitisha shughuli za uzalishaji, wakisubiri uamuzi wa
kamati iliyoundwa kushughulikia malalamiko yao kuhusu tozo mpya ya Sh 200,000
kwa kila gari linalotoka mgodini likiwa na mawe.
Hatua hiyo imechangiwa na kuanzishwa kwa tozo ya Sh200,000 kwa kila gari linalobeba mawe kutoka mgodini, jambo ambalo wachimbaji wanasema ni kubwa hailingani na hali halisi ya uzalishaji na gharama za uendeshaji.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji
Wilaya ya Shinyanga, Leonard Waziri, amesema kusimama kwa uchimbaji kumeathiri
si wachimbaji pekee bali pia shughuli nyingine za kiuchumi zinazotegemea sekta
hiyo katika eneo hilo.
Ameongeza kuwa ni muhimu serikali
kushughulikia kwa haraka suala hilo ili kupunguza mzigo wa tozo na kurejesha
mzunguko wa uchumi kwa wachimbaji na jamii inayowazunguka.
Mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro, alikutana na wachimbaji hao na kusikiliza malalamiko yao kabla ya kuunda kamati iliyojumuisha pande zote mbili wachimbaji na watalaam kutoka Halmashauri ili kupitia upya tozo hiyo na kufikia muafaka.

Mchimbaji mdogo wa madini,David Elias, amesema kusimama kwa uzalishaji kumezidisha hali ngumu ya kiuchumi kwa wachimbaji na kuomba serikali kuharakisha suluhisho ili kurejesha shughuli hizo muhimu.
Kwa upande wake, Janeth Ngangula amesema wachimbaji wako tayari kulipa tozo, lakini kiwango kilichowekwa ni kikubwa mno, na kusisitiza kuwa kamati iliyoundwa inapaswa kuharakisha mchakato wa kupitia upya tozo hiyo.
Naye Frank Moshi amependekeza kiwango hicho kipunguzwe hadi Sh20,000 kwa kila gari, akieleza kuwa kiwango hicho kinaweza kuendana na uhalisia wa uzalishaji na kuwapa wachimbaji nafasi ya kuendelea na shughuli zao.

Wachimbaji wadogo wa madini katika Mgodi wa Mwakitolyo, Halmashauri ya Shinyanga wamesitisha shughuli za uzalishaji, wakisubiri uamuzi wa kamati iliyoundwa kushughulikia malalamiko yao kuhusu tozo mpya ya Sh 200,000 kwa kila gari linalotoka mgodini likiwa na mawe.
Hatua hiyo imechangiwa na kuanzishwa kwa tozo ya
Sh200,000 kwa kila gari linalobeba mawe kutoka mgodini, jambo ambalo wachimbaji
wanasema ni kubwa hailingani na hali
halisi ya uzalishaji na gharama za uendeshaji.
Mchimbaji
mdogo wa madini,David Elias, amesema kusimama kwa uzalishaji kumezidisha hali
ngumu ya kiuchumi kwa wachimbaji na kuomba serikali kuharakisha suluhisho ili
kurejesha shughuli hizo muhimu.
Kwa upande wake, Janeth Ngangula amesema
wachimbaji wako tayari kulipa tozo, lakini kiwango kilichowekwa ni kikubwa mno,
na kusisitiza kuwa kamati iliyoundwa inapaswa kuharakisha mchakato wa kupitia
upya tozo hiyo.
Naye Frank Moshi amependekeza kiwango hicho
kipunguzwe hadi Sh20,000 kwa kila gari, akieleza kuwa kiwango hicho kinaweza
kuendana na uhalisia wa uzalishaji na kuwapa wachimbaji nafasi ya kuendelea na
shughuli zao.