WAHAMASISHWA KUWA WAZALENDO KWA MUSTAKABALI WA TAIFA

 
Vijana nchini wamehamasishwa kuwa wazalendo kwa nchi yao kwa kutambua nafasi yao muhimu katika kulinda na kuendeleza taifa, Wito huo unalenga kuwajenga kuwa na moyo wa kujituma, kuwajibika na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ili kuhakikisha nchi inaendelea kusonga mbele kwa mafanikio.
Imeeelzwa kuwa uzalendo ni msingi wa taifa imara, hivyo ni muhimu vijana kuanza kuujenga tangu wakiwa wadogo kupitia malezi na elimu sahihi,wanaweza kuelewa wajibu wao katika kulinda rasilimali za nchi, kuheshimu sheria na kudumisha amani iliyopo.

Hata hivyo, imebainika kuwa vijana wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusu historia ya nchi yao hali ambayo inafanya washindwe kujua taifa lilipotoka hadi lilipo sasa yakiwemo mafanikio makubwa yaliyopatikana .

Akizungumzia umuhimu wa vijana kujua historia ya nchi Chibura Makorongo mkazi wa Manispaa ya Shinyanga amesema,suala hilo linapaswa kupewa kipaumbele ili kuwasaidia kufahamu safari ya taifa na mchango wa waasisi wake Hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sherkhe Abeid Aman Karume.

Waasisi hao walifanya kazi kubwa kwa kuhakikisha wameweka msingi imara ambao umewezesha taifa kuendelea kuwa na amani,umoja na mshikamano hayo ni matunda ya viongozi hao ambao wataendelee kukumbukwa siku zote.

Sambamba na hilo, vijana wanapaswa kufundishwa kulinda na kuenzi tunu za taifa kama vile amani, mshikamano na umoja. Maadili haya yakizingatiwa kwa dhati yatawezesha kuendelea kuwepo kwa mazingira salama na yenye kuheshimiana miongoni mwa wananchi.

Akizungumzia suala la utandawazi na ujio wa sayansi na teknolojia amesema imekuja na mambo mengi yapo ya msingi na mengine yanachangia kuporomoka maadili katika taifa hasa kupitia kundi la vijana,ambapo amewashauri kuwa makini na kuzingatia mambo ambayo yanalinda utu na tamaduni zetu.

Post a Comment