Watanzania wametakiwa kusahau yaliyopita na kuelekeza nguvu zao katika kujenga taifa lenye mshikamano, upendo na maendeleo ya pamoja. Wito huo umetolewa ikiwa ni sehemu ya kuimarisha umoja wa kitaifa na kuhakikisha nchi inaendelea kusonga mbele kwa amani na utulivu.
Imeelezwa kuwa
kushikilia mambo ya zamani kunachangia kudhoofisha mshikamano wa jamii na
kuzuia juhudi za maendeleo, badala yake wananchi wanapaswa kuunganisha nguvu
zao na kuangalia mustakabali wa taifa kwa mtazamo chanya unaolenga ustawi wa wote.
Wito huo umetolewa na mwanasiasa Abdalla Sube mkazi wa Manispaa ya Shinyanga, amewaomba watanzania kuendeleza upendo miongoni mwao bila
kujali tofauti za rangi, dini au makabila,kwani taifa lenye watu
wanaothaminiana na kuheshimiana ndilo linaloweza kufikia maendeleo endelevu.
Pia amebainisha
kuwa ubaguzi wa aina yoyote unaweza kuwa chanzo cha migogoro na kuvuruga amani
iliyopo, hivyo kila mwananchi ana wajibu wa kulinda na kuimarisha mshikamano wa
kitaifa kwa vitendo.
Amesema watanzania tunatakiwa kushikamana, kupendana
na kusonga mbele kwa lengo la kuijenga nchi imara yenye umoja, amani na
maendeleo kwa kizazi cha sasa na kijacho na kusau mambo yaliyotokea nyuma.
Amesisitiza umoja na upendo kuwa ni msingi muhimu katika kuleta maridhiano
ya kweli ndani ya Jamii, wananchi wanapaswa kujenga tabia ya kusameheana,
kusikilizana na kuheshimiana ili kuondoa tofauti zinazoweza kuleta migawanyiko.
Kupitia mshikamano huo, jamii inaweza
kurejesha imani na kuimarisha uhusiano mzuri unaochochea maendeleo ya pamoja na
kujenga taifa linalozingatia utu na kuleta maridhiano kwa pande zote.
Amesisitiza kuwa maridhiano ya kudumu hayawezi
kupatikana bila kuwepo kwa moyo wa upendo na nia ya dhati ya kuishi kwa
amani,kwa kuzingatia misingi ya utu na kushirikiana katika shughuli za kijamii
na kiuchumi bila kubaguana, hali hiyo itasaidia kujenga taifa lenye utulivu,
mshikamano na lenye mwelekeo wa maendeleo endelevu.