Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Peter Masindi akifungua mafunzo ya madiwani wa Halmashauri hiyo yakuwajengea uwezo katika masuala ya maadili,rushwa na kukumbushwa wajibu wao ambayo yametolewa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga
Na Stella Herman,Shinyanga Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Peter
Masindi, amewataka madiwani kusimamia kwa umakini miradi ya maendeleo katika
maeneo yao huku akisisitiza kuwa wao ndiyo wawakilishi wa wananchi na nguzo
muhimu ya maendeleo ya Taifa.
Akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo madiwani
kuhusu kujiepusha na vitendo vya rushwa, kubaini mianya ya rushwa pamoja na
kuwakumbusha maadili na wajibu wao, Masindi amesema viongozi hao wanapaswa kuwa
chachu ya mabadiliko kwa kuwajibika ipasavyo katika maeneo wanayoyaongoza.
Amesema wananchi wanawategemea
madiwani kuwasimamia na kuwawakilisha vizuri, hivyo wanapaswa kuangalia
changamoto zilizopo katika kata zao na kuchukua hatua kwa wakati ili
kuhakikisha maendeleo yanapatikana.
“Wananchi watawapima baada ya miaka
mitano kwa kazi mtakazozifanya, Maendeleo ya kata yanawategemea ninyi,
msipofanya maamuzi sahihi kata zenu haziwezi kupata maendeleo,” amesema
Masindi.
Aidha amewataka madiwani kufanya
kazi kwa kuzingatia maadili, nidhamu pamoja na kutunza siri za vikao na
majukumu yao, akieleza kuwa dhamana waliyopewa ni kubwa ndiyo maana Serikali
imeamua kutoa mafunzo hayo ili kuwakumbusha wajibu wao kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni wakili Maximilian Kyabona, amewaasa madiwani kujiepusha kutanguliza maslahi binafsi mbele na kusahau kuwa wao ni wawakilishi wa wananchi.
Kyabona amesema madiwani ndiyo watakaowezesha Halmashauri ya Kishapu kupata maendeleo iwapo watawajibika ipasavyo, kupinga rushwa na kufichua mianya yote inayoweza kusababisha miradi ya maendeleo kushindwa kutekelezwa.
Alitaja baadhi ya mambo ambayo madiwani wanapaswa kuyaepuka kuwa ni pamoja na kubadili vifungu vya matumizi ya fedha, kuchukuliana posho pamoja na kujihusisha na zabuni mbalimbali zinazoweza kuleta mgongano wa maslahi.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Peter Masindi akifungua mafunzo ya madiwani wa Halmashauri hiyo yakuwajengea uwezo katika masuala ya maadili,rushwa na kukumbushwa wajibu wao ambayo yametolewa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu Josephat Limbe akizungumza wakati wa mafunzo kwa madiwani yaliyotolewa na TAKUKURU
Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu Maximilian Kyabona akitoa elimu ya masuala ya rushwa na maadili kwa madiwani wa Halmashauri ya Kishapu
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Kishapu Atuganile Stephen akifuatilia mafunzo ya madiwani
Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu Maximilian Kyabona akitoa elimu ya masuala ya rushwa na maadili kwa madiwani wa Halmashauri ya Kishapu
Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu Maximilian Kyabona akitoa elimu ya masuala ya rushwa na maadili kwa madiwani wa Halmashauri ya Kishapu
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Peter Masindi akifungua mafunzo ya madiwani wa Halmashauri hiyo yakuwajengea uwezo katika masuala ya maadili,rushwa na kukumbushwa wajibu wao ambayo yametolewa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga
Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu Maximilian Kyabona akitoa elimu ya masuala ya rushwa na maadili kwa madiwani wa Halmashauri ya Kishapu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu Josephat Limbe akizungumza wakati wa mafunzo kwa madiwani yaliyotolewa na TAKUKURU
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Kishapu Atuganile Stephen
amesema mafunzo hayo yamelenga kuwakumbusha madiwani wajibu wao pamoja na suala la maadili katika kusimamia miradi na kujiepusha kutanguliza mbele maslahi yao binafsi badala ya kuwatumikia wananchi waliowachagua.