KATAMBI AWEKA WAZI MIKAKATI YA MAENDELEO,AWASHUKURU WANANCHI KWA KUMPA RIDHAA TENA

Na Stella Herman, Shinyanga

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini  na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Patrobas Katambi ameahidi kuendelea kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo kwa kusimamia miradi ya maendeleo katika sekta za miundombinu, maji, afya, elimu na ajira kwa vijana.

Mhe. Katambi ameyasema hayo leo februari 22,2026  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Zima moto Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi ambapo amewashukuru  kwa kumchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo pamoja na kumchagua Rais Samia Suluhu Hassan.

Waziri Katambi amesema  kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii yanayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja ili kuhakikisha changamoto zinazowakabili wananchi zinakwisha.

Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii yanayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.

Katika hatua nyingine Mhe. Katambi amesisitiza suala la amani

 Kwa kuhakikisha wananchi kuwa wananchi wanakuwa salama na utulivu wa kutosha  Serikali itaendelea kuimarisha usalama wa raia na mali zao ili kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na ukuaji wa uchumi.

amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kumwamini na kumteua tena kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, akiahidi kuitumikia nafasi hiyo kwa uadilifu na kwa maslahi ya wananchi.

Katika hatua nyingine, Katambi amemuonya mkandarasi anayejenga stendi ya mabasi ya kisasa na barabara ya lami kuelekea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, akimtaka kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo au aachie kazi kabla hajachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa, amempongeza Katambi kwa kuendelea kuaminiwa na Rais, na kumtaka kushughulikia changamoto ya upatikanaji wa vitambulisho, vya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa kusogeza huduma katika ngazi ya kata. 

Ameahidi kuendelea kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo kwa kusimamia miradi ya maendeleo katika sekta za miundombinu, maji, afya, elimu na ajira kwa vijana, huku akieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii yanayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Patrobas Katambi akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa kwenye mkutano wa hadhara wa kuwashukuru kwa imani yao ya kumchagua kuwa Mbunge pamoja na kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM.


Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Patrobas Katambi akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa kwenye mkutano wa hadhara wa kuwashukuru kwa imani yao ya kumchagua kuwa Mbunge pamoja na kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Patrobas Katambi, akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano mkubwa wa hadhara Mjini Shinyanga, akitoa shukrani kwa imani waliyoionesha katika Uchaguzi Mkuu kwa kumchagua kuwa Mbunge, kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kuwachagua madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). 
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Patrobas Katambi, akihutubia wananchi wa Shinyanga katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru kwa imani yao ya kumchagua kuwa Mbunge pamoja na kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Patrobas Katambi, akihutubia wananchi wa Shinyanga katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru kwa imani yao ya kumchagua kuwa Mbunge pamoja na kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Patrobas Katambi, akihutubia wananchi wa Shinyanga katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru kwa imani yao ya kumchagua kuwa Mbunge pamoja na kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM.

Post a Comment