
Mwanafunzi mwenye mahitaji maalumu, Prisca Samson anayesoma katika Shule ya Wasichana Mkoani Geita, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kujenga na kuimarisha shule hizo, hatua ambayo imesaidia watoto wa makundi maalumu kupata fursa sawa ya elimu.
Prisca amesema kuwa ujenzi wa shule hizo umefungua milango kwa watoto wengi wenye mahitaji maalumu kupata elimu bora bila kubaguliwa.
Ameeleza kuwa sasa wana nafasi ya kuchaguliwa na kusoma katika mazingira rafiki yanayowawezesha kufikia ndoto zao.
Akizungumza kwa furaha katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, mwanafunzi huyo amesema anajivunia kumuona Rais Samia akiendelea kuwajali watoto wa makundi maalumu na kuhakikisha wanapata haki yao ya msingi ya elimu.
Witness, ambaye ana ndoto ya kuwa daktari siku zijazo, amesema kuwa msaada huo wa Serikali unawapa moyo na kuwahamasisha kusoma kwa bidii ili kutimiza malengo yao na kulitumikia taifa.

Amehitimisha kwa kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake unaojali makundi mbalimbali ya jamii, hususan watoto wenye mahitaji maalumu, na kuahidi kuwa ataendelea kusoma kwa bidii ili kufikia ndoto yake ya kuwa daktari.