
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalum, Dorothy Gwajima, amezindua mradi wa (PAMOJA) unaolenga kuongeza upatikanaji wa fursa za kiuchumi kwa wanawake na kuimarisha huduma za kutokomeza na kukabiliana na athari za ukatili wa kijinsia.
Uzinduzi wa mradi huo umefanyika leo wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Mkoa wa Geita.
Akizungumza baada ya uzinduzi wa PAMOJA, Waziri Gwajima amesema maadhimisho hayo ni fursa muhimu ya kutathimini mafanikio na michango ya wanawake katika maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Ameeleza kuwa kupitia mradi huo, wanawake watawezeshwa kiuchumi pamoja na kupata huduma na msaada wa kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoathiri ustawi wao na familia.
Katika hatua nyingine, Waziri Gwajima amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia utoaji wa mikopo yenye riba nafuu.
Amesema kuwa kupitia mpango huo, jumla ya shilingi bilioni 4.8 tayari zimetolewa kwa wanawake wa Mkoa wa Geita ili kuwasaidia kuanzisha na kuendeleza shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Gwajima amesisitiza kuwa uwezeshaji wa wanawake kiu
chumi ni hatua muhimu katika kuleta maendeleo endelevu na ustawi wa jamii.